HISTORIA YA GWIJI WA POP MICHAEL JACKSON


Michael Joseph Jackson alizaliwa mnamo tarehe 29 Agosti mwaka 1958 huko Gary, Indiana Marekani na kufariki dunia mnamo tarehe 25 Juni 2009.  Alikuwa mwimbaji, dansa na mburudishaji kutoka nchini Marekani. Hufahamika zaidi kwa jina la kiheshima au utani kama Mfalme wa Pop. Hutambulika kama mburudishaji aliyepata mafanikio zaidi kwa muda wote, na alikuwa ni mmoja kati ya waburudishaji wenye mvuto mkubwa kwa hadhira katika medani ya muziki. Michael ana mchango mkubwa katika soko la mziki duniani kote hasa katika dansi la jukwaani  na pia alipenda  kuanika hadharani maisha yake binafsi, imemfanya awe kioo cha ulimwengu katika tamaduni maarufu kwa ziaidi ya miongo minne .

Akiwa pamoja na ndugu zake, Michael alianza mziki kwa mara ya kwanza akiwa kama mwanachama mdogo kabisa katika kundi la The Jackson 5 mnamo mwaka wa 1964. Michael Jackson alianza kuonekana jukwaani akiwa na miaka mitano tu pamoja na kaka na dada zake. Alitokea familia ya wanamuziki ya Jackson Five. Kuhusu miaka yake ya awali alisimulia mara kadhaa ya kwamba baba alimlazimisha kufanya mazoezi mno ya kucheza na uimbaji hivyo Michael hakuufaidi kabisa utoto maana alikuwa akihudhulia majukwaani akiwa na umri mdogo zaidi na kulazimishwa kuishi kama mtu mzima na mashughuli akiwa na kundi lililokuwa likiratibiwa na baba yao mzazi mzee Jackson.
Baada ya mafanikio makubwa ya kundi hilo Michael alianza kujitegemea kama msanii binafsi mnamo mwaka 1971. Na  albamu yake bora kabisa aliitoa mwaka 1982 na kuipa jina la Thriller imebaki kuwa albamu yenye mauzo bora kwa muda wote duniani. Staili ya muziki wake, sauti na namna ya utumbuizaji  wake zilitambulika vizazi kwa vizazi na hata mavazi yake nayo yalivutia kwa rangi na hata mishono yake ya kipekee.

Michael ni mmoja kati ya wasanii wachache waliowekwa mara mbili kwenye tuzo za Rock and Roll Hall of Fame. Mafanikio mengine yanajumlisha kuweka record za guiness, Guinness World Records  ikiwa ni pamoja Mburudishaji Mwenye Mafanikio kwa Muda Wote, ameshinda tuzo za Grammy 15, ikiwa ni pamoja na ile ya Living Legend Award na ile ya Lifetime Achievement Award, 26 American Music Awards 24 akiwa kama msanii pekee wa kujitegemea, pamoja na moja kwa ajili ya Msanii wa Karne —zaidi ya msanii mwingine yeyote nyimbo zake 17 zimeshika nafasi ya kwanza huko nchini Marekani ikiwa ni pamoja na nne akiwa kama mwanachama wa kundi la Jackson 5, na inakadiriwa kafanya mauzo ya rekodi zaidi ya milioni 750 dunia nzima, na kumfanya kuwa miongoni mwa wasanii waliouza sana rekodi zao kwa muda wote na haijawahi kutokea tena.

Maisha binafsi ya Michael yalikuwa hayakaukiwi utata kwa miaka kadhaa moja ya utata huo ni kashifa za kujibadilisha kwa mwonekano wake hali hii ilianza kujidhihilisha mwishoni mwa miaka ya 1970 na kuendelea, Michael aliyezaliwa kwa maumbile ya Mwamerika mweusi mwishoni alikuwa na ngozi nyeupe usoni na baada ya upasuaji kadhaa pua yake ikawa nyembamba si pana tena. Mwenyewe  alijitetea kwa kusema kwamba badiliko la rangi lilisababishwa na ugonjwa. Ingawa hoja hiyo ilikosa mashiko kwa wasikilizaji na wafuatiliaji wa maisha yake na kuendelea kusababisha maswali mengi hasa kwenye vyombo vya habari na mashabaki wake.  

Mnamo mwaka wa 1993 Michael alishtakiwa kwa kosa la udhalilishaji wa kijinsia kwa watoto, ingawa hakukutwa na hatia baada ya uchunguzi kukamilika. Michael katika maisha yake amewahi kuoa mara mbili, kwanza alioa mnamo 1994 na akaja kuoa tena mnamo 1996. Na alibahatika kupata watoto watatu. Michael, alimwoa Bi. Lisa Marie Presley, binti wa Elvis Presley. Jackson, pia alikuwa akimiliki eneo kubwa lenye makazi lililoitwa Neverland, ambalo baadaye liliuzwa kwa kampuni na nusu bado inamilikiwa na mwenyewe.

Michael alifariki mnamo tar. 25 Juni 2009 kwa kuzidisha kiasi cha dawa za usingizi wakati anajiandaa na ziara ya tamasha lake la This Is It, ambalo lilitakiwa lianze katikati ya mwaka wa 2009. Iliripotiwa kwamba alitumia dawa aina ya propofol na lorazepam. Afisa uchunguzi wa vifo wa wilaya ya Los Angeles lieleza baada ya uchunguzi kuwa kifo chake kilisababishwa na daktari wake kutokuwa makini wakati akitoa dozi ya dawa kwa mteja wake na iliaminika kuwa hali hiyo ni sawa na uuaji. Na mashtaka yalielekezwa kwa daktari wake binafsi kwa kosa la kuua bila kukusudia. Kifo cha Jackson kilileta huzuni kubwa ulimwenguni kote hasa kwa wadau na wapenzi wa mziki wa pop. Mazishi yake yalitangazwa na kushirikisha watu wote duniani kote kwa njia mbali mbali huku maelfu ya watu wakihudhuria katika kuuaga mwili wake.

Michael Jackson maisha yake yalikuwa wazi sana na yaliwavutia wengi. Pia, alishawahi kukumbwa na kashfa ya  kwa unyanyasaji wa mtoto, lakini hakukutwa  na kosa. Alifanya upasuaji maalumu ili abadilishe mwonekano wake. Watu waliomtazama hawakupatana kama mabadiliko ya kimaumbile yalikuwa ama tokeo la kuona aibu kuonekana kama Mwafrika au jaribio kuwa na uso linalorahisisha mawasiliano yake na watu wa bara zote.

Na Emmanuel Venance.

HISTORIA YA GWIJI WA POP MICHAEL JACKSON HISTORIA YA GWIJI WA POP MICHAEL JACKSON Reviewed by Burudani Za Bongo on 01:16 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.