HISTORIA YA RUDY YOUNGBLOOD WA APOCALYPTO
Rudy Youngblood msanii,
mwanamziki, muigiza wa sanaa za maonesho na mwana ndondi. Rudy alizaliwa mnamo September 21 1981 huko Belton,Texas Marekani. Familia ya Rudy ilikuwa masikini mno maana majukumu
ya kuilea familia hiyo yenye watoto watatu ambao ni Rudy na dada zake wawili
ilikuwa chini ya mama yao na baba yao hakuwepo. Kulingana na umasikini wa
familia yao, Rudy alianza kujihusisha na
shughuli za ujenzi akiwa na umri wa miaka kumi tu. Alianza kuwasaidia mafundi
ili angarau ajipatie kipato kitakachomsaidia mama yake katika kuiendesha
familia yao nahii ikawa fursa kwake ya kujifunza ufundi ujenzi na uselemala
wakati akifanya kazi kama msaidizi wa mafundi.
Rudy alibahatika kusoma kwenye
shule ya serikali ambayo ni Belton High School hii ni miongoni mwa shule za watu masikini na
alipenda sana mchezo wa masumbwi alipokuwa shuleni hapo, Rudy alikuwa ni
mshindani mzuri na mchapa makonde maarufu shuleni kwao. Pamoja na kupenda
masumbwi lakini Rudy alikuwa shabiki wa sinema
hivyo alihudhulia mara kwa mara kwenye majumba ya sinema na kujikuta
akipenda zaidi kuigiza. Baada ya kuhitimu masomo ya sekondari anapata bahati ya
kuhuzuria masomo kwenye chuo cha sanaa za maonesho alikwenda kusomea ngoma za
asili na sanaa za maonesho ambazo ndizo alizipenda zaidi. Alishiriki maoneso
mbalimbali na kikundi cha American Indian Dance Theatre.
Baada ya maonesho kadhaa anapata nafasi ya kufanya usahili wa kushiriki
kwenye sinema na hapo ndipo, Rudy anafanikiwa kuchaguliwa kuwa mmoja wa washiriki
katika filamu ya The Seventh Fire.
Na mwaka mmoja baadae anakuwa mhusika mkuu
kwenye filamu ya Apocalypto. Iliyosimamiwa
na Los Angeles Times. Rudy anachaguliwa na mwandishi na Mwongozaji maarufu wa
sinema hiyo bwana Mel Gibson ili ashiriki kama Jaguar Paw katika sinema hiyo. Rudy
ni mhindi mwekundu kwa asili na mhusika alihitajika kuwa mhindi mwekundu. Rudy
ilimlazimu kuchukua muda kujifunza lugha ya Yucate Maya ambayo ndiyo ilitakiwa
kuzungumzwa na wahusika kwenye sinema hiyo ya Apocalypto na miswada yote
iliandikwa kwa lugha hiyo.
Filamu alizoshiriki mpaka sasa ni American
Mythos, Crossing Point, Shepherd's Blade, Wind Walkers, Amnesia, Beatdown,
Apocalypto, Spirit: The Seventh Fire, Hook Up. Pia alishiriki katika filamu ya
Beatdown na Into the Americas. Rudy anakadiliwa kuwa na ukwasi wa dora 500,000.
Rudy amewahi kukumbwa na masahibu kama vile kukamatwa na polisi akiwa amelewa chakali
lakini aliwahi kukumbwa na kashifa ya kuwapiga wacheza kamali wenziye mwaka kwenye
kasino moja huko marekani mnamo mwaka 2017.
Rudy hapendi kutumia mitandao ya kijamii kabisa
pamoja na kuwa kwenye muongo wa mitandao ya kijamii na karibu watu mashuhuri na
maarufu kote duniani kutumia mitandao hii swala hili limekuwa tofauti kabisa
kwa Rudy maana hana akaunti facebook, twitter, instagram, snapchap, wala telegram.
HISTORIA YA RUDY YOUNGBLOOD WA APOCALYPTO
Reviewed by Burudani Za Bongo
on
05:10
Rating:
Reviewed by Burudani Za Bongo
on
05:10
Rating:


No comments: